Leo March 15, 2018 Msemaji wa familia ya Tundu Lisu amesema ni kweli awali Lisu alikuwa akiishi kwa wasamaria wema baada ya kuruhusiwa alipokuwa akitibiwa kabla ya kurudishwa tena kwa ajili ya matibabu ya goti.
Akizungumza na vyombo vya habari Alute Mugwhai ambaye ni kaka yake na Lisu amesema, wanaendelea kusubiri kuhusu suala la matibabu na uchunguzi wa tukio lakupigwa risasi kwa Tundu Lisu na kwamba endapo hawatajibiwa watajipanga kuchukua hatua wenyewe wakiwa kama familia.