Leo March 12, 2018 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imekwama kusikiliza ushahidi wa kesi inayomkabili Ofisa Msaidizi wa Forodha wa (TRA), Jennifer Mushi anayedaiwa kumiliki magari 19 yenye thamani ya Sh.Mil 197.6 yasiyolingana na kipato chake kwa sababu mashahidi wamepata udhuru.
Wakili serika Peter Vitalis amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa lakini mashahidi wamepata udhuru.
Wakili Vitalis amedai kuwa mashahidi wamepangiwa majukumu mengine na waajiri wao na wametoa udhuru, hivyo kesi iahirishwe hadi tarehe nyingine.
Baada ya kueleza hayo Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi April 9,2018.
Katika kesi hiyo, mshtakiwa anadaiwa kati ya March 21, 2016 na June 30, 2016 maeneo tofauti ya Jiji la Dar es Salaam, akiwa mfanyakazi wa TRA alikutwa akimiliki mali zisizolingana na kipato chake, kinyume na sheria.
Inadaiwa alikutwa akimiliki magari 19, yakiwemo Toyota Rav4,Toyota dyna truck, Toyota viz, Suzuki carry na Toyota Ipsum yote yakiwa na thamani ya Mil.197,601,207
Pia anadaiwa kati ya March 21, 2012 na March 30, 2016 maeneo ya Dar es salaam akiwa mwajiriwa wa TRA aliishi maisha ya kipato cha juu (kifahari) tofauti na kipato chake yenye thamani ya sh.Mil 333,255,556.24.
“HATA WAKIANDAMANA NDANI YA NYUMBA, MTU AKAUMIA, ALIYEITISHA ATAWAJIBIKA” WAZIRI MWIGULU