Taarifa niliyoipokea muda mfupi uliopita inahusu maamuzi ya baraza la madiwani manispaa ya Kinondoni jijini Dar es salaam kuwasimamisha kazi watumishi wawili akiwemo mwanasheria Mkuu wa Manispaa hiyo kwa kuiletea Serikali hasara ya Bilioni 7.
Akizungumza na ITV, Mstahiki Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob ameeleza mambo kadhaa ambayo yamepelekea watumishi hao kusimamishwa, baadhi ya mambo aliyoyaeleza ni pamoja na haya………
>>>’wamekiuka maagizo ya Rais John Magufuli ambayo mwaka jana akiongea na wafanyabiashara Ikulu alionyesha nia ya kutoliachia eneo la Coco beach lakini kwa makusudi watu wetu wa sheria bado hawajakata rufaa na hawana chochote wanachoangaika nacho’
>>>‘zamani mwenge stand tulikuwa tunapata milioni 12 kwa mwezi lakini baada ya uwekezaji wa makumbusho tunapata milioni 4 kwa mwezi tunapoteza fedha nyingi sana pamoja na uwekezaji wa jengo ambalo halina mkataba na manispaa, Jengo hilo la ghorofa hatuna makubaliano na halipo kwenye document ya manispaa tunachunguza kuangalia fedha zilikuwa zinaenda mfukoni kwa nani’
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE
ULIIKOSA YA MUSOMA KIVUKO KUKOSA HONI MIEZI MIWILI? BONYEZA PLAY HAPA CHINI