Habari za kuongezeka kwa ukusanyaji wa mapato katika Taasisi nyingi za Serikali zinazidi kuchukua vichwa vya habari, tuliona Jeshi la Polisi Usalama Barabarani na sehemu nyingine mapato yakiongezeka. Leo Tarehe 11 March 2016 Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi nao wameingia kwenye list ya ukusanyaji mapato mengi kwa kipindi kifupi.
Wizara hiyo imekusanya mapato ya mil 676.4 kuanzia December 19 2015 hadi March 9 2016, makusanyo haya yameongezeka baada ya Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi William Ole Nash kuagiza Idara za Huduma za Mifugo na uzalishaji na masoko kufanya doria ili kuhakikisha kwamba mifugo yote ambayo inanunuliwa kwenye minada ya awali inapelekwa kwenye mnada wa upili uliopo Pugu Dar es salaam ili kukaguliwa afya zao na kutolewa ushuru.
Ambapo hapo awali wafanyabiashara walikuwa wakikwepa kupeleka mifugo yao ili kukwepa ushuru wa Serikali, akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara, Mkurugenzi wa Huduma za mifugo, Abdu Hayghaimo amesema..
>>>’Baada ya kuanza kazi za doria na kudhibiti maeneo yote kuanzia machinjioni hadi kwenye mnada wa pugu, mapato ya Serikali kwenye mnada wa pugu yamepanda kwa wiki kutoka wastani wa sh mil 24 mwezi December 2015 kwa wiki hadi sh mil 61 kwa wiki mwezi March 2016′
>>>‘hii inaonesha kwamba kabla ya doria kulikuwa na upotevu mwingi wa mapato ya Serikali kwenye mnada wa Pugu na kwenye machinjio ya Mkoa wa Dar es salaam‘
ULIIKOSA HII VIDEO WAKATI WAZIRI NCHEMBA AKIFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA USIKU NA KUMFUKUZA KAZI MKURUGENZI? TAZAMA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.