Ujenzi wa majengo ya ghorofa yaliyo chini ya kiwango yaliripotiwa katika jiji la Dar es salaam miaka ya nyuma iliyopita ambapo kariakoo kulikuwa na ghorofa 64, taarifa nyingine ilikuwa ni ya jengo la ghorofa kuporomoka na kusababisha vifo vya watu kadhaa.
April 06 2016 Bodi ya Wakandarasi imemfikisha Mahakamani Kisutu Dar es salaam mfanyabiashara na Mwanasiasa Thomas Ngawaiya kwa kosa la kufanya shughuli za ujenzi wa jengo la hoteli lenye thamani ya zaidi ya MILIONI 500 Kinondoni Dar es salaam bila kutumia wakandarasi waliosajiliwa.
Mtuhumiwa yuko nje kwa dhamana ambayo amedhaminiwa na wadhamini wawili ambapo masharti yake kila mmoja awe na ahadi ya MILIONI 250 na hati ya nyumba.
Akizungumza baada ya kesi hiyo Mwanasheria wa Bodi ya usajili wa makandarasi, Saddy Kambona amesema….>>>’Mtuhumiwa ameshtakiwa kwa kutokutumia wakandarasi waliosajiliwa kama ambavyo sheria ya bodi ya makandarasi namba 17 ya 1997 na ilipofanyiwa 2008 inavyotaka kwamba majengo yote ya matumizi ya umma lazima yajengwe kitaalamu na wakandarasi waliosajiliwa kwa hiyo shughuli hizo za ujenzi zimekuwa zikiendelea bila kuwepo kwa wakandarasi waliosajiliwa badala yake umekuwa unafanywa na mafundi wa kawaida tu’.
Upelelezi wa kesi hiyo bado unaendelea na kesi imeahirishwa na itatajwa tena April 21 2016.
ULIIKOSA YA JENGO LA GOROFA 16 LILILOJENGWA KIMAKOSA DAR KUBOMOLEWA? ANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE