Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
Moja ya yalioandikwa ni huu utafiti kwenye gazeti la Mwananchi chenye kichwa ‘Mende ni dawa ya vidonda vya tumbo’.
#MWANANCHI Baada ya kubainika maziwa ya mende yana protini imeelezwa miguu yake hutumika kwa matibabu ya binadamu pic.twitter.com/TYkY3nAkrs
— millardayo (@millardayo) August 1, 2016
Baada ya uchunguzi wa kisayansi kubaini kwamba maziwa ya mende yana protini mara nne zaidi ya maziwa ya ng’ombe na kifaru, imebainika kwamba maziwa ya mende pia hutumika kwa matibabu mbalimbali ya binadamu.
Miongoni mwa matibabu hayo ni pamoja na kutengeneza miguu bandia ya kutumiwa na binadamu, mtafiti mkuu katika mradi uliofanyika katika Chuo Kikuu cha A&M cha Texas Hong Liangnchini Marekani amesema…….>>> ‘Nilipoona hii kwa mara ya kwanza nilishangaa’
Alisema wanasayansi kwa miaka mingi wamekua wakishangazwa na uwezo wa mende wa kukaa muda mrefu maeneo yenye sumu na uchafu bila kudhurika, wamegundua kwamba huwa wanatoa kemikali za kupambana na sumu.
Wanaweza kusaidia katika kutengeneza dawa za kusaidia binadamu kukabiliana na bakteria wanaoathiri zaidi watu kwa mfano E.Coli na MRSA ambao hawauliwi kwa dawa yoyote.
Hii siyo mara ya kwanza mende kuhusika kwenye matibabu, Mwandishi Lafcdio Hearn Karne ya 19, alipitia maeneo ya kusini mwa Marekani na kuripoti jinsi watu wenye pepopunda walivyokua wakipewa chai iliyotengenezwa kwa kuwekwa kwa mende aliandia kuwa …….>>>’Sijui ni mende wangapi hutumiwa hadi upate kikombe cha chai, lakini wakazi wa New Orleans wana imani na tiba hiyo’
Pia alisema China kuna mafuta yanayotengenezwa kwa kutumia ungaunga wa mende. Hutumiwa kutumiwa vidonda vya moto pia humezwa kutibu vidonda tumbo. Kuna aina 4500 ya mende na aina nne pekee ambao huwa waaribifu.
#MWANANCHI Wawili wakutwa wamefariki gesti, Gongo la Mboto Dar huku miili yao ikiwa imeungua moto pic.twitter.com/9N7pCy7h4U
— millardayo (@millardayo) August 1, 2016
#MWANANCHI Picha aliyopiga Senga ikionyesha askari wakimpiga na hatimaye kumuua Mwangosi yatawala ibada ya kumuaga pic.twitter.com/BI8uaZhWWa
— millardayo (@millardayo) August 1, 2016
#MWANANCHI JPM apiga marufuku usafirishaji wa mchanga wa madini kwenda nje na kuagiza ujenzi wa viwanda hapa nchini pic.twitter.com/pKVGAGzl7Q
— millardayo (@millardayo) August 1, 2016
#NIPASHE Lowassa asema pamoja na kukatwa jina lake CCM lakini JK hakufanikiwa kumpitisha chaguo lake kwenye vikao pic.twitter.com/kOXm4c2DON
— millardayo (@millardayo) August 1, 2016
#NIPASHE Waliohusika na mauaji ya mfanyabiashara Seif Athuman na Koplo Milambo, TMK, Dar wahukumiwa kunyongwa pic.twitter.com/H17DHqW7Yf
— millardayo (@millardayo) August 1, 2016
#MWANANCHI Pacha waliotenganishwa Mbeya wasumbuliwa na tatizo la kutokwa na haja kubwa na ndogo bila wao kujitambua pic.twitter.com/MHCy7Mn1S5
— millardayo (@millardayo) August 1, 2016
#MWANANCHI CHADEMA imesema haitotekeleza mpango wa kuhamia Dodoma kwani ni wa kukurupuka pic.twitter.com/lu5zmuxeXR
— millardayo (@millardayo) August 1, 2016
#MWANANCHI Waziri Mhagama kupeleka kikosi kazi Dodoma ili kuandaa miundombinu ya barabara na nyumba za watumishi pic.twitter.com/vnlgYgqIEY
— millardayo (@millardayo) August 1, 2016
#JamboLEO Lowassa azungumzia utendaji wa JPM, asema kiongozi huyo anahitaji ushauri ili aweze kufikia malengo yake pic.twitter.com/MNhNcG4fPX
— millardayo (@millardayo) August 1, 2016
#MTANZANIA TPA yaboresha miundombinu ya bandari ya Mtwara ili kunufaika na fursa kubwa zilizopo mikoa ya kusini pic.twitter.com/YzcHZam7Wn
— millardayo (@millardayo) August 1, 2016
#HabariLEO Rais Magufuli acharuka, aagiza bodi ya pamba kuondoka Dar kuhamia mikoa ya kanda ya ziwa pic.twitter.com/6MhssGSEe0
— millardayo (@millardayo) August 1, 2016
ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI AUGUST 1 2016 KUTOKA AYO TV? UNAWEZA KUIANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI