Headline za kuungua kwa majengo katika jiji la Arusha zimeendelea tena leo August 21 2016 ambapo katika kata ya Lemara mama mmoja anayejulikana kwa jina la Victoria Edward Wenga amechoma moto maduka yanayokadiriwa kuwa manne na nyumba yake ya kuishi.
Millardayo.com imempata Diwani wa kata ya Lemara Prof. Raymond Mosha ambapo amesema chanzo cha mama huyo kuchoma moto inadaiwa ni ugomvi uliokuwepo kwenye familia kati ya mama huyo na mume wake anayejulikana kwa jina la Edward Wenga.
Katika tukio hilo imeelezwa kuwa mtu mmoja amejeruhiwa na mali zote zimeteketea kwa moto.
ULIKOSA HII AJALI YA GARI DOGO ILIYOTOKEA KATI YA MATAA YA MLIMANI CITY NA TCRA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI