Jumatano ya August 23 mchezo wa ngao ya hisani wa watani ya jadi kati ya Simba dhidi ya Yanga ulichezwa uwanja wa Taifa, huo ni mchezo amba0 unaashiria ufunguzi wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2017/2018, Ligi ambayo itaanza weekend hii.
Mchezo kati ya Simba na Yanga huo ulikuwa ni mchezo wenye ushindani mkubwa, hususani kipindi hiki timu hizo zikiwa zinakutana wakati huu baada ya kukamilisha usajili wa vikosi vyao, ugumu wa mchezo huo huo na presha ya mashabiki uliifanya game hiyo dakika 90 imalizike kwa sare 0-0.
Baada ya dakika 90 kumalizika kwa 0-0 muamuzi wa kati Ely Sasii aliitisha mikwaju ya penati na Simba kufanikiwa kushinda kwa mikwaju ya penati 5-4, huku nahodha wao msaidizi Mohammed Hussein “Tshabalala” akikosa penati na Juma Mahadhi na Kelvin Yondani wakikosa penati kwa upande wa Yanga.
Ushindi huo wa leo wa Simba dhidi ya Yanga katika mchezo wa Ngao ya Hisani unakuwa ni Ubingwa wao wa tatu wa Hisani toka ilipoanzishwa mwaka 2001 wakati Yanga wao wamechuku mara tano, Simba walichukua Ngao hiyo 2011 kwa kuifunga Yanga 2-0 na 2012 kwa kuifunga Azam FC 3-2.
VIDEO: Ushindi wa Simba vs Rayon Sports, Simba Day 8 2017 Full Time 1-0