Taarifa iliyotolewa leo September 15 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, imeeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Mhandisi Emmanuel Korosso kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL).
Taarifa hiyo imesema kuwa uteuzi wa Mhandisi Emmanuel Korosso unaanza mara moja. Mhandisi Emmanuel Korosso anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Salim Msoma ambaye alimaliza muda wake.
Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Mhandisi Ladislaus Ernest Matindi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL). Kabla ya uteuzi huu Mhandisi Ladislaus Ernest Matindi alikuwa Mkurugenzi katika Shirika linaloshughulikia masuala ya usafiri wa anga Barani Afrika (EGNOS-Africa Joint Programme Office) lenye makao yake nchini Senegal.
ULIKOSA HII YA RAIS MAGUFULI KUSEMA WANALALAMIKA PESA ZIMEPOTEA…HII MSG IENDE CLEAR KWAO? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI