Kazi ya millardayo.com ni kuhakikisha unakuwa huru kufanya mambo yako kama kazi na masomo kisha ukitulia unakutana na kila kubwa la kila muda kwa sababu kazi yangu ni kuhakikisha hupitwi na chochote mtu wangu.
Hii hapa chini ni ripoti ya ripota wa nguvu Simon Simalenga akiwa Dodoma (104.4 CloudsFM) na hii ni ripoti kuhusu mazito yaliyojitokeza ikiwemo baadhi ya Wabunge kuhoji uwezo wa Profesa Anna Tibaijuka kikazi.
Bonyeza play kusikiliza hapa chini
Hata hivyo jioni hiohiyo ya May 28 2014 bungeni wakati bajeti ya Wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya Makazi ikimiliki headlines, waziri mkuu Mizengo Pinda alilazimika kuingilia kati kuinusuru bajeti hiyo iliyokuwa katika hatari ya kukwama kutokana na wabunge kadhaa kushika shilingi katika mshahara wa Waziri wakitaka ufafanuzi wa kina kuhusu hoja tofauti ikiwemo ya mji mpya wa Kigamboni na suala la mabaraza ya ardhi.
Huku mbunge wa Kigamboni Dr. Faustine Ndugulile (CCM) akiongoza kutoa hoja nzito kuhusu mpango usioeleweka wa Waziri Tibaijuka na wizara yake, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alikiri kutokushirikishwa kwa wananchi wa Kigamboni katika mchakato wa ujenzi mji mpya Kigamboni hivyo akaahidi kuanza upya kwa mchakato huo kwa kuwashirikisha wananchi na baraza la madiwani katika hatua zote.
Ili niwe nakutumia kila taarifa inayonifikia jiunge na mimi kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Instagram facebook na kupata pichaz, video, stori na mengine yote ya hii dunia.