Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG imeamplfy kwamba kitendo cha Serikali kukosa nyaraka za mali zake kumechangia baadhi ya watendaji wasio waaminifu kutumia mwanya huo kujisogezea mali za umma.
Katika ripoti yake ya Ukaguzi kwa mwaka 2013 CAG Ludovick Utouh amesema ofisi yake imebaini upotevu wa magari 11 yaliyonunuliwa kwa ajili ya matumizi na mamlaka ya maendeleo na biashara Tanzania (TanTrade) ambayo hadi sasa hayafahamiki yalipo.
Ofisi yake inalifanyia uchunguzi suala hilo na tayari imegundua hayo magari yalisajiliwa kwa namba binafsi badala ya namba za serikali huku akisema ‘wizara ya viwanda na biashara ilinunua magari kwa ajili ya bodi ya biashara na tunaomba kusema magari hayo tumejaribu kuyafatilia lakini hayaonekani na hayajulikani yalipo na ni magari mapya yalinunuliwa kwa ajili ya TanTrade lakini TanTrade wenyewe wanasema hawajayapokea na Wizara inasema haijui yako wapi’
Kwenye sentensi nyingine kamati ya kudumu ya bunge serikali za mitaa LAAC imesikitishwa na kitendo cha halmashauri ya jiji la Mwanza kupata hati chafu za hesabu kwa mwaka 2013 na kupanga kwenda kufanya uchunguzi juu ya kilichochangia kutokea kwa hiyo ishu.
Mwenyekiti wa LAAC Rajabu Mbaruku amesema kamati yake imepata upinzani ilipotaka kukagua hesabu za halmashauri hiyo baada ya watendaji wake kukimbia ofisi zao kwa hiyo kamati ikashindwa kufanya mahojiano na ukaguzi katika jiji la Mwanza.
‘Sasa tutakapoanza shughuli zetu mkoa wa kwanza utakua Mwanza
Spika wa Bunge ametangaza kupanga ratiba ili kutoa fursa kwa ripoti hiyo ya hesabu za serikali kwa mwaka ulioshia June 30 2013 kujadiliwa na wabunge.
Unataka stori kama hizi zisikupite? jiunge na ripota wako wa nguvu kwenye twitter instagram na facebook kwa jina hilohilo la @millardayo