Wema Abraham Sepetu ni mrembo mwenye headlines zake nyingi TZ kwa zaidi ya miaka 10… toka amekuwa Miss Tanzania, akaingia kwenye filamu na nyingine mpya kabisa ni safari yake kuingia kwenye headlines za siasa !!
Alikuwa LIVE kwenye show ya Clouds360 leo June 24 2015, mengine mapya kumi ambayo nimeyapata toka kwake ni haya hapa mtu wangu.
Unaijua ratiba yake ya kila siku; “Huwa naamka saa mbili au saa tatu inategemea na nini natakiwa kufanya siku hiyo… nafanya kazi za nyumbani kama mwanamke mwingine, napenda sana kupika. Nikiwa niko nyumbani sina kazi yoyote ninakaa na kupika.. kitu kinachochukua sana muda wangu ni shooting ya reality show na movie, sipendi sana kutokatoka”>>> Wema Sepetu.
Hii ndio sababu iliyomsukuma akaona agombee Ubunge; “Nimezaliwa kwenye siasa, Marehemu baba yangu alikuwa ni mwanasiasa, mama yangu ni mwanasiasa mpaka sasa hivi ni Mwenyekiti wa Serikali za mitaa. Marehemu baba yangu aliwahi kuniambia kwamba anatamani niingie kwenye siasa, mwaka 2010 nilikuwa siko tayari.. nimejisikia vibaya baba yangu amefariki wakati sijaonesha kwamba ninaweza kufanya, nina uhakika kule aliko anajisikia fahari”>>>
Kwanini kagombea Singida?; “Mama yangu ametoka Singida, nimeona hiyo ndio sehemu nzuri ya kwenda kugombea na huu ndio muda sahihi… nadhani ninaweza kujitolea kwa jamii yangu kwa sababu Singida ni nyumbani“>>> Wema Sepetu.
Akipata Ubunge nafasi ya kwanza ni yeye na wanawake; “Kipaumbele change itakuwa ni wanawake, kwa sauti yangu na ushawishi wangu ninajua kwamba nitaweza”
Vipi akiangalia anaona upepo umekaa vizuri? “Upepo uko vizuri… Nilikuwa Singida wiki iliyopita na ninarudi wiki ijayo.. nitakuwa nafanya ziara ili wapate kuniona. Singida mimi ni maarufu sana kwa sababu ya mama yangu anatokea kule, kwa hiyo wanahitaji kumuona mtoto wao… Huwezi kujiwekea asilimia 100 kwamba utashinda lakini unatakiwa kuweka 75% kwamba utashinda… nafarijika kwa jinsi wanavyonipokea. Wasanii tuna nafasi nzuri kwa sababu tunafahamika” >>> Wema Sepetu.
Vipi kuhusu ile clip ya sauti ambayo imezagaa mitandaoni? “Nilivyoisikia kwa mara ya kwanza nilikuwa na mama yangu, nilijisikia vibaya sana. Ile sauti sio yangu kabisa”
Akiingia kwenye Ubunge vipi kuhusu usanii? ; “Siwezi kuacha sanaa kwa sababu ya Ubunge, nilikuwa na shughuli zangu kabla ya Ubunge, siwezi kusema ninaacha kabisa kila kitu kwa sababu ya Ubunge” >>>
Sauti yote ya Wema Sepetu iko hapa, unaweza kuchukua time yako kusikiliza kila kitu cha kwake ndani ya dakika 30.
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook naInstagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.