Ilianza kama ishu ya kawaida hivi lakini muda ulivyozidi kwenda ikazidi kuchukua headlines kwenye mitandao ya kijamii kwamba eti kuna watu wananunua sarafu za shilingi mia tano za Tanzania alafu wanatumia madini ya sarafu hiyo kutengeneza vito kama mikufu hivi !
Nimepitia kwenye channel ya Youtube ya blogger mkubwa Tanzania, Issa Michuzi >>>Michuzi TV na nimekutana na hii stori nikaona niisogeze hapa kushare na wewe pia.
Anayehojiwa ni Abdul M. Dollah ambaye ni Meneja Msaidizi wa Huduma za Kibenki Benki Kuu TZ… Majibu yake ni haya kuhusu hiyo ishu; “Huu uvumi tumeusikia wananchi wengi wanakuja na kuulizia habari hiyo, huo ni uvumi tu na sio kweli kwamba kuna madini yoyote katika hii sarafu ya mia tano ambayo yanaweza kutengeneza vito vya thamani” >>> Abdul M. Dollah
“Wakati tunaizindua hii sarafu mwaka jana tuliwaambia kwamba humu ndani kuna madini ya chuma kwa asilimia 94 na madini ya Nikel asilimia sita tu… Benki Kuu inaamini kwamba Wananchi wanadanganywa” >>> Abdul M. Dollah
Video ya Interview hiyo nimekuwekea hapa pia, ukiplay utayapata majibu yote kutoka BoT.
https://www.youtube.com/watch?t=11&v=HEN55I5DKDM
Jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.