Kizungumkuti cha usajili barani Ulaya kimeanza kushika kasi huku timu zikijiandaa kwa ajili ya msimu mpya wa soka barani ulaya.
Miezi kadhaa iliyopita klabu ya soka ya Chelsea ilithibitisha rasmi kwamba haitomuongezea mkataba mpya mchezaji Ashley Cole ambaye alijiunga na timu hiyo mwaka 2003 akitokea Arsenal. Baada ya taarifa hiyo timu nyingi zikaanza kuhusishwa na usajili wa mchezaji huyo.
Leo hii imethibitishwa rasmi kwamba mchezaji huyo amejiunga rasmi na timu ya AS Roma ya Italia.
Cole ambaye alikuwa akilipwa mshahara wa Paundi 185,000 kwa wiki na Chelsea imekubali kupata kiasi cha £160k kwa makubaliano ya kulipwa kiasi kisichozidi £35,000 kwa wiki na klabu hiyo ya Serie A.
Ashley Cole amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo ya Rome.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta FB