Kwenye Kikao cha Bunge jana JUNE 29 2015 Naibu Spika Job Ndugai alimwomba Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage atoe ufafanuzi kuhusu ujumbe uliosambazwa kwa message na Mitandaoni kwamba kuna mgomo wa kuuza mafuta ya petroli na dizeli.
Naibu Waziri akajibu kwamba ni uvumi usio na ukweli wowote, leo Mbunge wa Ubungo, John Mnyika akawasha kipaza sauti na kuirudisha hiyo ishu tena >>>”Nimesimama kutoa hoja kwamba shughuli za Bunge ziweze kusitishwa ili tuweze kwa ajili ya kujadili hoja ya dharura ambayo ina athari kwa nchi na lina maslahi kwa umma.
Jana Naibu Waziri wa Nishati na Madini juu ya tetesi za mgomo wa mafuta katika majibu yake alihakikisha kwamba hakuna mgomo, niliyasikiliza majibu ya Waziri nikiwa Dar es Salaam.
Nilipotoka Dar kuja Dodoma, kuanzia natoka Ubungo nimefanikiwa kupata mafuta mbele kidogo ya Kibaha… Ukweli ni kwamba kulikuwa na mgomo, vituo vyote nilivyosimama wanasema hawana mafuta>>>- John Mnyika.
Viko vituo vilivyogoma kuuza na viko vichache sana vinavyouza vimeamua kupandisha bei, naomba shughuli za Bunge zisitishwe na tujadili jambo hili>>>- Mbunge John Mnyika.
Akapewa nafasi Naibu Waziri wa Nishati na Madini >>> “Tunayo mafuta ya kutosha kati ya siku 12 mpaka siku 40, hatuna tatizo na kuna meli ziko kwenye maji zinakuja… ninaihakikishia nchi hii kwamba haiwezi kutokea tatizo.
Nawatuma Wakaguzi Tanzania nzima muache tuwatafute, ukikutwa umekataa kuuza mafuta faini ni milioni 20 na unaweza ukafungiwa kituo. Hii ndio kazi niliyosomea muache watu waje kufaidi, ndio maana jana niliwaambia kichaa karogwa tena… nilikuwa Mkaguzi sasa hivi ni Waziri muache nifanye kazi.
Watanzania muwe na amani soko lina mafuta, huyo aliyetuma message atakamatwa na tutampatia adhabu anayostahili, Bunge liendelee hii shughuli iko katika mikono salama” >>>- Naibu Waziri Charles Mwijage.
Tukubaliane kuna mambo ambayo yanawaumiza Watanzania kwa pamoja, tusikae tukatengeneza jambo hili na siasa ndani yake… Maeneo mengine ukienda unaangalia kwenye visima unakuta hamna mafuta. Kama tatizo ni la kutengenezwa litakwisha, na kama lina namna nyingine yoyote Meli ziko Baharini , zitakuja na litakwisha” >>>- Naibu Waziri wa Fedha, Adam Kigoma Malima.
Naibu Spika wa Bunge akafunga mjadala >>> “Sioni sababu kulihusisha Bunge na jambo ambalo litakwisha kesho kwa sababu bei ya leo na kesho itakuwa tofauti kwa sababu ya dola… Bila EWURA kutangaza bei mpya hatuwezi kumaliza tatizo hili.
Kama hali itaendelea kuwa mbaya kesho na keshokutwa tutasema hili tulijadili, namini litaisha haraka sana” >>> — Job Ndugai.
Hapa ninayo sauti niliyorekodi Bungeni Dodoma leo June 30 2015, bonyeza play usikilize ishu yote ilivyokuwa.
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook naInstagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.