Watu wa Kenya wanahesabu wiki tatu kabla ya kuishuhudia siku ambayo walikuwa wakiisubiri kwa hamu, ugeni wa ‘ndugu yao’ Rais wa Marekani, Barack Obama… Sarah Obama ni bibi yake Obama, amekutana na Gavana wa Nairobi na kugusia kuhusu uwezekano wa Obama kutembelea Kijijini kwao, Kogelo
Balozi wa Marekani Kenya amesema bado hawajapanga Safari ya Obama atatembelea wapi na wapi mpaka sasa.
“Mama Sarah amenithibitishia kwamba Rais Obama atatembelea Kijijini kwao kuona Kaburi la Baba yake“, aliongea mmoja wa watu ambao walikuwa karibu na bibi yake Obama.
Matumaini yao wanaamini ujio wake una neema, Shule zitakarabatiwa, barabara zimeanza kukarabatiwa na mengine mengi mazuri yatawafikia pia.
Ninayo hii stori ya K 24 hapa mtu wangu, ina ripoti yot kuhusu kinachoendelea Kenya kuhusu ujio wa Obama.
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.