Headlines zimeendelea kwenye mwaka huu wa Uchaguzi 2015 ambapo UKAWA sio jina geni kwa Watanzania, vyama mbalimbali vya upinzani vikiwemo CHADEMA na C.U.F vilijiunga na vinataka kumtangaza mgombea mmoja atakaewawakilisha.
Zitto Kabwe ambaye aliondolewa kwenye chama cha CHADEMA, alijiunga na chama cha A.C.T Wazalendo March 2015 ambapo siku kadhaa baadae chama hicho kilitaka kujiunga na UMOJA WA KATIBA YA WANANCHI (UKAWA) lakini imeshindikana, haya hapa chini ndio maneno ya Zitto Kabwe July 26 2015.
‘Leo siku nzima nilikua nina kikao cha mashauriano na viongozi wa chama wa kata zote za mkoa wa Dar es salaam ( mikutano mikuu ya majimbo 10 ya Dar) jumla ya wajumbe 1023 walihudhuriam, tumesisitiza kuwa hatutajiunga UKAWA… ikumbukwe kuwa tuliomba utaratibu wa kujiunga UKAWA mwezi Aprili mwaka 2015 na hatujajibiwa rasmi lakini moja ya chama ndani ya UKAWA kilitangaza kuwa hawatutaki‘ – Zitto Kabwe
‘Hata juzi kwenye gazeti la Mawio waliandika kuwa tumefukuzwa UKAWA, sisi tumeamua kuingia kwenye uchaguzi wenyewe.. tarehe 10 Agosti 2015 tutatangaza mgombea Urais tutakayemuunga mkono baada ya mkutano mkuu wa kidemokrasia wa ACT Wazalendo.
Tutanadi #AzimioLaTabora kama zana ya kuleta mapinduzi katika nchi yetu‘- Zitto
Kwenye sentensi nyingine ya Facebook aliyoandika Zitto Kabwe saa kadhaa kabla ya hiyo ya juu aliandika >>> #ACTWazalendo Tutaingia kwenye uchaguzi wenyewe. We will go it alone as a party to defend our principles. Mkutano Mkuu wa Chama wa Kidemokrasia ( National Convention) utafanyika tarehe 10 Agosti 2015′
Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.