Kampuni ya Adidas imesema kuwa inatarajia kupoteza dola Bilioni 1.3 mwaka huu kutokana na kushindwa kuuza nguo na viatu vya brand ya “Yeezy” ya Rapper Ye (Kanye West) ambaye ilivunja mkataba naye October 2022 kutokana na matamshi ambayo Kampuni hiyo iliyaita ya chuki dhidi ya Wayahudi.
Adidas imesema mwenendo wa mapato ya Kampuni hiyo kwa mwaka 2023 umechangiwa na kutokuuza bidhaa za “Yeezy” walizonazo kwa sasa.
Kwa upande mwingine, Kampuni hii imesema inaweza kujaribu kuuza nguo hizo zikiwa zimeondolewa chapa ya “Yeezy” ambapo kama watafanya hivyo basi itawasaidia kuokoa takribani dola milioni 300 za kampuni hiyo.