Ishu ya mizigo ya abiria kupimwa uzito kabla ya kupakiwa kwenye Ndege ni kawaida, mambo yamegeuka… Uzbekistan wanapima mpaka uzito wa abiria mtu wangu!!
Shirika la Ndege la Uzbekistan limezigonga tena headlines kubwa duniani baada ya Shirika hilo kutangaza kwamba wanaleta utaratibu ambao na abiria nao itabidi wapimwe uzito kabla ya kupanda ndege, na hii sio kwa maana mbaya… wanaamua kufanya hivi kama hatua ya kuchukua tahadhari kabla ya kuanza safari ili wajue kabisa uzito ambao umepakiwa kwenye ndege.
Wamesema uzito wa mtu itakuwa ni taarifa ya siri ambayo ni kwa ajili tu ya usalama wa Ndege zao kwenye safari, hautaoneshwa mahali popote, japo hawajasema watafanya nini ikitokea uzito wa abiria na mizigo utazidi kwenye kiwango kinachotakiwa kwenye Ndege.
Nimejaribu kucheki mitandaoni na kukuta kumbe hii ya Uzbekistan sio mpya.. Samoa Air ni Shirika le Ndege lililopo nchi ya Samoa, waliwahi kuutumia utaratibu wa kupima uzito abiria ambapo ikitokea mtu amezidi uzito anatozwa bei sawasawa na bei ambayo anatozwa abiria akizidisha uzito wa mzigo… na malipo hayo ni nje kabisa ya nauli ambayo umeilipia.
Unaambiwa kwenye Ndege za Samoa Air waliweka mpaka siti za watu waliozidi uzito wa Kilo 130 ambazo zilipewa jina la ‘Samoa XL’, siti pana zaidi kuliko nyingine za kawaida.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos