Naambiwa December 11 2015 ndio itakua siku yenyewe ya Viongozi/Wafanyabiashara na Taasisi mbalimbali kupewa tuzo za kutambua mchango wao kwenye ishu mbalimbali walizozifanya kitofauti katika kuleta mabadiliko kwenye jamii ya Watanzania.
Ni tuzo ambazo zitagusa mpaka makampuni ambayo yanamiliki Mabango yanayotumika kutangaza biashara mbalimbali barabarani, vituo vya TV, Magazeti yaliyofanya vizuri pamoja na taasisi nyingine.
Hii ni mara ya kwanza kwa Taasisi na Makampuni mbalimbali ya Tanzania kutunukiwa tuzo ambapo kupata details zaidi unaweza kuwafatilia Tanzania Leadership Awards kwenye Twitter Facebook na Instagram >>> @TZAwards