Headlines kuwepo kwa wingu zito huko China zilichukua nafasi katika vyombo mbalimbali vya habari na kusababisha Serikali kuagiza baadhi ya viwanda vifungwe kwa siku kadhaa ili kukabiliana na hali hiyo.
Kingine kilichonifikia kuhusiana uchafuzi wa hali ya hewa ni kwamba kuna mgahawa ambao umeamua kuwatoza wateja wake fedha kwa ajili ya kupata hewa nzuri wanapokua katika eneo lao.
Mgahawa huo ulioko Mashariki mwa China, katika mji wa Jiji la Zhangjiagang, unatoza wateja wake kiasi cha Yuan moja ambazo kwa pesa ya Tanzania ni kama shilingi 333 ili waweze kupata hewa safi wanapopata huduma ndani ya mgahawa huo.
Kiasi hicho cha pesa kinachopatikana kinatumika kuendesha kiyoyozi AC na mashine ya kusafisha hewa ndani ya mgahawa.
Kumekuwa na tatizo la maeneo mbalimbali ya China kusambaa kwa ukungu mkubwa unaotokana na mabadiliko ya tabia nchi yanayochochewa na hewa nzito inayotoka viwandani ambapo kuna baadhi ya viwanda vimelazimika kufungwa kwa muda.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE