Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu yaTwitter >>>@millardayo.
Najua huenda stori nyingine zinakupita, hapa nimezikusanya zote zilizoguswa na #Tweets za #Magazeti Desemba 18, 2015, unazisoma zote kwa pamoja.
Vigogo wa TRA wanaokabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kutokana na upotevu wa makontena 329 wameachiwa kwa dhamana #MWANANCHI #DEC18
— millard ayo (@millardayo) December 18, 2015
Wasomi wamesema moja ya vitu Serikali inapaswa kufanya ili kukusanya mapato mengi ni pamoja na kuziba mianya ya rushwa #MWANANCHI #DEC18
— millard ayo (@millardayo) December 18, 2015
Mkaguzi wa Hesabu CAG adaiwa kukiuka maagizo ya Rais MAGUFULI, asafiri nje ya nchi na kutumia Mil.15 kwa siku tatu #MagazetiDEC18 #MTANZANIA
— millard ayo (@millardayo) December 18, 2015
Spika wa Bunge Job NDUGAI amesema afya yake ni njema na anaendelea na majukumu yake kama kawaida #MTANZANIA #DEC18 >>https://t.co/sE9eylYINh
— millard ayo (@millardayo) December 18, 2015
Wizara ya ardhi jana ilitekeleza ubomoaji nyumba zaidi ya 100 zilizojengwa kwenye bonde la mto Msimbazi na kusababisha vilio #MWANANCHI DEC
— millard ayo (@millardayo) December 18, 2015
Waziri wa afya Ummy Mwalimu amesema atamwomba Rais MAGUFULI amwajibishe endapo atashindwa kumaliza tatizo la dawa za saratani #MWANANCHI DEC
— millard ayo (@millardayo) December 18, 2015
Jaji Mark BOMANI amesema njia pekee ya kumaliza mgogoro wa Z’bar ni kuunda jopo maalum #MagazetiDEC18 #MTANZANIA >>https://t.co/sE9eylYINh
— millard ayo (@millardayo) December 18, 2015
Siku moja baada ya CHADEMA kuahirisha ziara za LOWASSA mikoani, chama hicho kimesema hakitambui zuio la maandamano kutoka kwa IGP #MTANZANIA
— millard ayo (@millardayo) December 18, 2015
DC Paul Makonda amekerwa na malipo ya tata ya bilioni 5.7 kwa ajili ya ujenzi wa barabara 6 zilizojengwa kwenye Wilaya yake #MWANANCHI DEC18
— millard ayo (@millardayo) December 18, 2015
Chuo kikuu cha tiba IMTU kimepewa siku 14 kuhama eneo la Mbezi Beach kutokana na kushindwa kulipa kodi ya bilioni 3 #MagazetiDEC18 MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) December 18, 2015
Mawaziri wafanya ziara ktk taasisi na idara mbalimbali na kutoa maagizo kudhihirisha uwepo wao #Magazeti #MTANZANIA >https://t.co/sE9eylYINh
— millard ayo (@millardayo) December 18, 2015
Jumla ya wanafunzi laki 5 waliofaulu mtihani wa darasa la saba wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza ktk shule za Serikali #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) December 18, 2015
Mwanasheria mkuu mstaafu Mark Bomani ameitaka Serikali kuendeleza mchakato wa kupata katiba mpya ulioanzishwa na JK mwaka 2012 #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) December 18, 2015
Wachina wanaokabiliwa na kesi ya kukutwa na pembe 11 za faru zenye thamani ya mil.900 wamehukumiwa jela miaka 20 na faini bil.10 #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) December 18, 2015
Waziri wa Madini Prof.Muhongo ameagiza bodi ya bonde la mto Rufiji kuwafungia maji wakulima wenye mashamba makubwa ya umwagiliaji #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) December 18, 2015
Babu wa Samunge ataka Rais MAGUFULI awahakikishie wananchi huduma bora za afya, asema muujiza mkubwa zaidi utakaovutia uko njiani #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) December 18, 2015
Mkuu wa Wilaya ya Kaliua, Tabora na wenzake watatu wakutwa na kesi ya kujibu ya ubadhirifu wa zaidi ya bilioni 3 za pembejeo #MWANANCHI DEC
— millard ayo (@millardayo) December 18, 2015
Mameya wa Manispaa Mwanza wameagiza kupatiwa orodha ya nyumba zitakazobomolewa #MagazetiDEC18 #MTANZANIA >>https://t.co/sE9eylYINh
— millard ayo (@millardayo) December 18, 2015
RC Geita ameagiza kusimamishwa kazi Muhandisi wa Halmashauri kupisha uchunguzi wa tuhuma za kuisababishia Serikali hasara kubwa #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) December 18, 2015
Kundi la wabunge wa Kenya limetoa wito kwa viongozi wa nchi za EAC kuchukua hatua kusuluhisha mgogoro wa Burundi #MagazetiDEC18 #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) December 18, 2015
Mume amuua mkewe kwa panga kutokana na wivu wa mapenzi kisha na yeye kujinyonga kwa kamba Mbeya, aacha ujumbe wa kumlaumu mkewe #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) December 18, 2015
Wanafunzi 12,000 waliofaulu kwenda Sekondari hawatoanza masomo kutokana na kutokamilika kwa madarasa TZ #MTANZANIA >>https://t.co/sE9eylYINh
— millard ayo (@millardayo) December 18, 2015
Mahakama ya Wilaya Chato imesema maofisa 6,Mkuu wa Wilaya Khadija NYEMBO wana kesi ya kujibu kwenye sakata la ubadhirifu pembejeo #TzDAIMA
— millard ayo (@millardayo) December 18, 2015
Rais MAGUFULI maarufu ‘tingantinga’ ameng’oa visiki ndani ya Serikali yake kwa muda mfupi na kuibua mjadala ndani na nje ya nchi #Jamboleo
— millard ayo (@millardayo) December 18, 2015
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.