Klabu ya Man United ambayo kwa kawaida imezoeleka kuingia na kufanya vizuri katika michuano ya klabu Bingwa barani Ulaya, kiasi hata cha kuwa inafikia hatua ya fainali ya michuano hiyo, kwa sasa inashiriki michuano ya UEFA Europa Ligi ambapo imecheza usiku wa February 25 na kuibuka na ushindi.
Man United waliwakaribisha klabu ya FC Midtjylland katika hatua ya timu 32 bora katika dimba la Old Trafford, nakufanikiwa kuwafunga kwa jumla ya goli 5-1, ushindi ambao magoli yalisababishwa na Nikolay Bodurov kujifunga goli la kwanza dakika ya 32, ikiwa ni dakika 5 zimepita toka Pione Sisto aipatie goli la kwanza FC Midtjylland.
Baada ya FC Midtjylland kujifunga Man United walikuja juu na kupachika magoli manne kupitia kwa Marcus Rashford dakika ya 63 na 75, Ander Herrera kwa mkwaju wa penati dakika ya 87 ikiwa ni penati ya pili ya Man United kupata katika mchezo huo, baada ya Juan Mata kukosa penati ya kwanza dakika ya 43. Memphis Depay akapachika goli la mwisho dakika ya 90.
Video ya magoli ya mech ya Man United Vs FC Midtjylland
https://youtu.be/5YC2_KoQAC8
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE