Usiku wa May 11 2016 wakati wa mkutano wa 38 wa shirikisho la soka barani Afrika chini ya Rais wake Issa Hayatou umetangaza mabadiliko katika mashindano ya ngazi ya vilabu barani Afrika, katika hotuba ya Issa Hayatou ameeleza mpango wa kubadilisha mfumo wa michuano ya Klabu Bingwa Afrika na shirikisho.
Kuanzia mwaka 2017 mashindano ya Klabu Bingwa barani Afrika CAF yatakuwa yanashirikisha Makundi manne baada ya mawili kama mfumo wa sasa unavyofanya, mabadiliko hayo hayajaishia katika mashindano ya Klabu Bingwa Afrika pekee hata Kombe la shirikisho barani Afrika.
Mkutano huo wa 38 wa CAF umefanyika Mexico katika mji wa Mexico na kuhudhuriwa na Rais wa sasa wa shirikisho la soka Duniani FIFA Gianni Infantino akipewa sapoti na Samuel Eto’o, Luis Figo na Zvonimir Boban ambapo manguli hao wa soka wamealikwa na FIFA kwa ajili ya shughuli itakayofanyika uwanja wa Azteca Mexico.
ALL GOALS: MBEYA CITY VS YANGA MAY 10 2016, FULL TIME 0-2
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE