Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
Moja ya yalioandikwa ni huu utafiti kwenye gazeti la Nipashe chenye kichwa ‘Njia rahisi kufyeka vitambi ni hii’
#NIPASHE Imebainika kuwa njia nyingine ya kukabiliana na tatizo la kitambi ni kunywa maji kwa wingi pic.twitter.com/Sf731fDEJs
— millardayo (@millardayo) July 30, 2016
Wakati maelfu ya watu duniani kote wakitambua kuwa njia maarufu ya kukabiliana na tatizo la kitambi na uzito mkubwa ni kuzingatia lishe bora na kushiriki mazoezi, imebainika kuwa njia nyingine ya kukabiliana na tatizo hilo ni kunywa maji kwa wingi.
Ripoti ya utafiti uliofanyika hivi karibuni juu ya uhusiano juu ya kiwango cha maji mwilini na uzito mkubwa, imefichua kuwa watu wazima wenye kawaida ya kunywa maji kwa wingi au kula vyakula venye majimaji mengi huwa na uwezekano mdogo wa kupata vitambi na kuwa na uzito mkubwa usiolingana na maumbile ya miili yao. Utafiti huo uliohusisha watu wazima takribani 10,000.
Kiongozi wa utafiti huo Dk Chang, ambaye ni profesa msaidizi katika Chuo Kikuu cha shule ya Afya Michigan nchini Marekani amesema…….>>>‘Wale wote ambao hutumia maji kwa kiasi kidogo walikutwa na uzito mkubwa zaidi kwa kipimo cha ulinganifu wa uzito wa mwili-BMI’s kulinganisha na wale ambao hunywa maji ya kutosha’
SOURCE: NIPASHE
Unaweza kupitia hapa habari nyingine kubwa kwenye magazeti ya Tanzania
#MWANANCHI Baada ya utafiti kubaini wingi wa protini ktk maziwa ya mende serikali yasema haina mpango na maziwa hayo pic.twitter.com/uKzE1gs9Ul
— millardayo (@millardayo) July 30, 2016
#MWANANCHI Rais Magufuli amesema watakaong'ang'ania Dar pic.twitter.com/j60ppvfel4
— millardayo (@millardayo) July 30, 2016
#MWANANCHI Spika Ndugai amerejea nchini kutoka India alikokwenda kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa afya yake pic.twitter.com/LEwXg0TpIV
— millardayo (@millardayo) July 30, 2016
#MWANANCHI Zaidi ya watoto mil 77 duniani hawanyonyeshwi ndani ya saa 1 baada ya kuzaliwa na kukosa kinga za mwili pic.twitter.com/3MtIwWDyOx
— millardayo (@millardayo) July 30, 2016
#MWANANCHI RC Rugimbana amezitaka wizara, taasisi za Serikali kusubiri siku 14 ili utolewe utaratibu wa kuhamia Dom pic.twitter.com/hKqvbadCPl
— millardayo (@millardayo) July 30, 2016
#NIPASHE Baada ya serikali kutangaza mchakato wa kuhamia rasmi Dodoma hofu imetanda juu ya kuibuka utapeli, uhalifu pic.twitter.com/XzwYFjg2pg
— millardayo (@millardayo) July 30, 2016
#NIPASHE Wadaiwa bodi ya mikopo ya elimu ya juu kuchukulia hatua ikiwemo kufikishwa mahakamani pic.twitter.com/gE9r7mUaJJ
— millardayo (@millardayo) July 30, 2016
#HabariLEO Muhimbili kuanza kupandikiza vifaa vya kuongeza usikivu kwa watoto na figo kuanzia mwakani pic.twitter.com/LCSwxeeBe1
— millardayo (@millardayo) July 30, 2016
#MWANANCHI Mahakama imetupilia mbali mapingamizi yaliyowekwa na wagombea ubunge wa CCM Jimbo la Mlimba na Kilombero pic.twitter.com/4NHgzWdKyx
— millardayo (@millardayo) July 30, 2016
#JamboLEO Rais Magufuli awakunjulia makucha CHADEMA, asema yeye ni tofauti, hajaribiwi pic.twitter.com/nA9aRqDX8p
— millardayo (@millardayo) July 30, 2016
#JamboLEO Ukata umeelezwa kusababisha kuyumba biashara ya baa Dar, baadhi zafungwa, zingine zapunguza wafanyakazi pic.twitter.com/rBwqgxjLt1
— millardayo (@millardayo) July 30, 2016
#NIPASHE Vigogo wenye vyeti bandia presha juu, baadhi wadaiwa kujisalimisha kwa waganga wa kienyeji pic.twitter.com/gBNfg9uaEn
— millardayo (@millardayo) July 30, 2016
ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI JULY 30 2016 KUTOKA AYO TV? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI.