Chama cha soka nchini Uingereza FA May 16 kimetangaza adhabu kwa vilabu vya Chelsea na Tottenham amabavyo vinatoka jiji moja la London, FA wametangaza uamuzi wa kuvipiga faini vilabu hivyo kutokana na kushindwa kuwadhibiti wachezaji wake kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu.
FA imetangaza kuipiga faini Chelsea ya pound 375,000 ambazo ni zaidi ya Tsh bilioni 1 ya kitanzania, wakati klabu ya Tottenham Hotspurs imepigwa faini ya pound 225,000 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 700 za kitanzania, maamuzi yamefanyika kutokana na wachezaji wa timu hizo kufanyiana vitendo visivyo vya kinidhamu wakati wa mchezo dhidi yao.
Mechi hiyo ambayo ilichezwa Stamford Bridge ilimalizika kwa sare ya goli 2-2, lakini muamuzi alitoa jumla ya kadi za njano 12, hata hivyo mapema mwezi huu Dembele wa Tottenham alifungiwa mechi sita kutokana na kumpelekea vidole Diego Costa wa Chelsea machoni kwa makusudi.
TUKIO LA DEMBELE ALILOMFANYIA DIEGO COSTA WAKATI WA MCHEZO HUO
https://youtu.be/HfoJjgLYlCQ
WACHEZAJI WA YANGA WALIVYOKABIDHIWA KOMBE LA LIGI KUU WAKIWA NA FAMILIA ZAO MAY 14 2016
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE