Mshambuliaji wa kimataifa wa Misri anayeichezea Liverpool ya England Mohamed Salah ameendeleza kuwa na msimu mzuri katika Ligi Kuu England akiwa na Liverpool licha ya kuwa hakufanya vizuri sana akiwa Chelsea mwaka 2014-2016.
Mohamed Salah ambaye wiki kadhaa zilizopita amefanikiwa kushinda tuzo ya PFA ya mchezaji bora wa mwaka wa Ligi Kuu England, leo amefanikiwa kuingia kwenye headlines mpya baada ya kutangazwa mshindi wa tuzo ya FWA ya mchezaji bora wa mwaka.
Baada ya ushindi wa tuzo ya FWA MO Salah mbaye anakaribia kuifikia rekodi ya Ruud van Nisterlrooy ya kufunga magoli 44 kwa msimu, ndio anakuwa mchezaji wa kwanza Afrika kuwahi kushinda tuzo hiyo lakini anakuwa mchezaji wa 15 kuwahi kushinda tuzo ya FWA na PFA kwa pamoja.
Salah pia ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza EPL kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa EPL mara nne katika msimu mmoja lakini pia ni mchezaji wa kwanza wa Liverpool kushinda tuzo ya FWA baada ya Steven Gerrard aliyestaafu na Luis Suarez aliyehamia na FC Barcelona.
Mapokezi ya Serengeti Boys baada ya kuwasili Tanzania na Kombe