Mchezaji wa zamani na aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya Nigeria Super Eagles Stephen Keshi amefariki dunia, taarifa za Keshi kufariki dunia zimeingia kwenye headlines kuanzia asubuhi ya June 8, habari ambazo mwanzo ilionekana kama tetesi ila baadae mitandao mikubwa kama The Mirror wa Uingereza ulithibitisha taarifa hizo.
Keshi mwenye umri wa miaka 54 amefariki ikiwa ni miezi michache imepita toka ampoteze mke wake December 2015 Kate aliyekuwa na umri wa miaka 35 kwa ugonjwa wa kansa, taarifa zinazoripotiwa kutoka ndani ya familia kuwa Keshi hakuwa na dalili zozote za kuumwa ila inaonekana ni kama mtu aliyekuwa na msongo wa mawazo kwa kumpoteza mkewe.
Afrika itamkumbuka Stephen Keshi kwa rekodi yake ya kuwa mwafrika wa pili kufanikiwa kutwaa taji la mataifa ya Afrika akiwa kama mchezaji na baadae kama kocha, wa kwanza kufanya hivyo alikuwa ni Mahmoud El-Gohary wa Misri. Nigeria pia itamkumbuka Stephen Keshi kama kocha pekee mzawa aliyefanikiwa kuwapa Kombe la Mataifa ya Afrika 2013.
ALL GOALS: TAIFA STARS VS MISRI JUNE 4 2016, FULL TIME 0-2
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE