Siku moja baada ya michezo ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kuchezwa na kushuhudia vilabu kadhaa vikiaga mashindano hayo, usiku wa April 14 ilikuwa ni zamu ya kushuhudia robo fainali ya michuano ya UEFA Europa league.
Miongoni mwa michezo iliyokuwa inatazamwa usiku wa April 14 ni mchezo kati ya Liverpool dhidi ya Borrusia Dortmund uliyochezwa katika dimba la Anfield, mchezo huo ulimalizika kwa Liverpool kuibuka na ushindi wa goli 4-3, hivyo kuiondoa Dortmund kwa aggregate ya 5-4.
Magoli ya Dortmund yalifungwa na Henrik Mkhitaryan dakika ya 5, Pierre-Emerick Aubameyang dakika ya 9 na Marco Reus dakika ya 57, wakati magoli ya Liverpool yalifungwa na Divock Origi dakika ya 48, Philippe Coutinho dakika ya 66, Mamadou Sakho dakika ya 78 na Dejan Lovren dakika ya 90.
Liverpool wameendeleza rekodi yao ya kutofungwa na vilabu vya Ujerumani ndani ya uwanja wao wa Anfield, kwani rekodi kutoka 101greatgoals zinaonesha Liverpool hajawahi kufungwa katika uwanja wao wa nyumbani na vilabu vya Ujerumani katika jumla ya mechi zake 13 alizocheza kabla ya mchezo huu. Sevilla, Shakhtar Donetsk na Villarreal ndio zimefuzu nusu fainali.
Video ya magoli ya Liverpool vs Dortmund
https://youtu.be/CmJuVDb5m7w
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE
VIDEO YA MAGOLI YA MECHI YA YANGA VS MWADUI FC, FULL TIME 2-1