Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ametoa futari kwa Taasisi, Mashirika na Jamii ya Mkoa huo ambapo amewaomba Waislam kupitia funga yao waombe na kukemea roho ya mauaji inayoendelea Mkoani humo.
Katika futari hiyo iliyohudhuliwa na Viongozi mbalimbali wa kidini na RC Mwanri ametaja aina nne za mauaji yanayojitokeza katika Mkoa wake na amekemea vikali kwa jamii inayochukua sheria mkononi “Mauaji katika Mkoa wa Tabora yana sura nne, wivu wa kimapenzi, kulipiza kisasi, ujambazi na ushirikina”
MLINZI WA SHULE AHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA, MAMA AANGUA KILIO