Mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina anayeichezea klabu ya FC Barcelona ya Hispania Lionel Messi, leo July 6 2016 jina lake limeingia kwenye headlines baada ya hukumu ya kesi yake ya ukwepaji kodi kutoka.
Lionel Messi amehukumiwa miezi 21 jela kutokana na kosa la ukwepaji kodi, hukumu hiyo ya Lionel Messi imetoka kutokana na kosa la kutuhumiwa kukwepa kodi pamoja na baba yake mzazi Jorge Messi kati ya mwaka 2007 na 2009, kiasi cha dola milioni 4.5 ambazo ni zaidi ya Tsh bilioni 9.8.
Hata hivyo kwa mujibu wa sheria za Hispania kwa watu wanaohukumiwa kifungo cha chini ya miaka miwili yaani mtu anaweza kutumikia kifungo chochote cha chini ya miaka miwili nje ya gereza.
UKWELI KUHUSU TAARIFA ZA MBWANA SAMATTA KUHAMIA AS ROMA UKO HAPA CHINI KWENYE HII VIDEO.