Usiku wa July 6 2016 michuano ya mataifa ya Ulaya 2016 maarufu kama Kombe la Euro, ilirejea tena baada ya kusimama kwa siku mbili kwa ajili ya mapumziko, usiku wa July 6 2016 ulichezwa mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya Euro 2016 kwa kuzikutanisha timu za taifa za Ureno dhidi ya Wales.
Ureno ambayo mara ya mwisho kufungwa na Wales ilikuwa May 12 1951 katika mchezo wa kirafiki, ilifanikiwa kuitoa Wales kwa kuifunga jumla ya goli 2-0, magoli ya Ureno yalifungwa kuanzia dakika ya 50 na Cristiano Ronaldo kwa kichwa, kabla ya dakika 3 baadae Luis Nani kupachika goli la pili kwa kutumia vyema assist ya Ronaldo.
#MillardAyoUPDATES #LiveMatch dk ya 80 #Portugal 2 (#Ronaldo 50′ #Nani 53′) -0 #Wales #EURO2016 pic.twitter.com/l19kgki5uL
— millard ayo (@millardayo) July 6, 2016
Kwa ushindi huo Cristiano Ronaldo ambaye ndio mchezaji bora wa mechi hiyo, anakuwa amefikia rekodi ya ufungaji bora wa muda wote iliyokuwa inashikiliwa na Michael Platini ya kufunga jumla ya magoli 9, Ronaldo ana nafasi ya kuvunja rekodi hiyo kama katika mchezo wa fainali atakaocheza na mshindi kati ya Ufaransa na Ujerumani kufunga goli moja.
#MillardAyoUPDATES #LiveMatch dk ya 67 #Portugal 2 (#Ronaldo 50′ #Nani 53′) -0 #Wales #EURO2016 pic.twitter.com/9WlZOpCOPn
— millard ayo (@millardayo) July 6, 2016
GOLI LA MECHI YA YANGA VS TP MAZEMBE JUNE 28 2016, FULL TIME 0-1