August 6 2016 wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya Kombe la shirikisho barani Afrika klabu ya Dar es Salaam Young Africans, walishuka katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam kucheza mchezo wao wa kirafiki dhidi ya klabu ya Mtibwa Sugar ya Manungu Morogoro.
Huo ni mchezo ambao Yanga wameutumia kujiandaa michezo yao miwili ya Kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya MO Bejaia na TP Mazembe, wakati Mtibwa huo ulikuwa mchezo wao wa maandalizi ya Ligi Kuu Vodacom Tanzania bara inayotaraji kuanza August 20 2016, hata hivyo mchezo umemalizika kwa 0-0, licha ya jitihada za timu zote kusaka goli.
Kufuatia sare hiyo Yanga leo August 6 anakuwa ametimiza jumla ya siku 73 toka apate ushindi wa mwisho katika mechi zake zake, ushindi wa mwisho Yanga kupata ilikuwa katika mchezo wa fainali ya Kombe la FA May 25 2016, baada ya kuifunga Azam FC kwa jumla ya goli 3-1 toka hapo ni siku 73 zimepita bila kupata ushindi katika mechi 5 zilizofuatia hadi sasa.
ALL GOALS: YANGA VS TP MAZEMBE JUNE 28 2016, FULL TIME 0-1