Usiku wa October 9 2016 wakati wa mchezo wa kuwania kufuzu kucheza Kombe la Dunia 2018 Urusi, kati ya timu ya taifa ya Hispania dhidi ya Albania, jina la beki wa FC Barcelona na timu ya taifa ya Hispania Gerard Pique lilirudi kwenye headlines baada ya kusemwa kuwa amekata michirizi ya bendera ya Hispania katika jezi yake.
Wengi walikuwa wanaamini kuwa Pique amekata mikono ya jezi hiyo iliyokuwa na michirizi ya bendera za Hispania kwa sababu ya harakati zake za kuunga mkono jimbo la Catalunya katika kudai uhuru wake wa kujitenga na Hispania, shirikisho la soka Hispania limetoa statement kuhusu madai ya mashabiki kwa Pique.
“Gerrard Pique aliikata mikono jezi yake ya mikono mirefu ili acheze akiwa comfortable kitendo ambacho huwa kinafanywa na wachezaji wa timu mbalimbali, jezi aliyovaa Pique ilikuwa ya mikono mirefu kama ilivyokuwa kwa Sergio Ramos na michirizi ya rangi za bendera ya Hispania huwa ipo katika jezi za mikono mifupi pekee”
ALL GOALS: Yanga vs Simba October 1 2016, Full Time 1-1