Siku 21 baada ya msanii wa Bongofleva Nuh Mziwanda atangaze kufunga ndoa na mchumba wake, December 1 2016 ndoa yao imeingia kwenye headlines mpya ambazo awali zilianza kuenea kama tetesi tu.
Nuh Mziwanda na mpenzi wake walifunga ndoa November 10 2016 huku tetesi zikiwa zimeenea mtaani kuwa wameamua kufunga ndoa baada ya mchumba wa Nuh Mziwanda kupata ujauzito.
Kupitia account ya instagram ya Nuh Mziwanda leo ameamua kupost picha na mkewe ikimuonesha kuwa ni mjamzito, picha ameipost na kuweka caption hii “Ukielewa maisha ni nini na unapaswa uweje ili uheshimike raha sana ‘Nawapenda sana Mashabiki wangu ❤️
VIDEO: Ulikosa kuona Shilole na Nuh Mziwanda walivyokutanishwa live kupitia TV? bonyeza play hapa chini