Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayeichezea klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta, amekubali kufanya exclusive interview na Ayo TV na kueleza maisha ya soka ndani ya timu ya KRC Genk anayoichezea.
Tumewahi kusikia headlines nyingi kuhusiana na wachezaji soka barani Ulaya kupangiwa aina ya vyakula wanavyotakiwa kutumia, Ayo TV imempata Samatta na kueleza utaratibu kwa timu yake kuhusu maswala ya vyakula kwa wachezaji.
“Suala la mtu kupangiwa chakula hilo halipo ila ushauri baada ya kufanyiwa vipimo utapewa, labda wewe unatakiwa ule chakula chenye protini nyingi au fat, mimi nilipopimwa wakati najiunga na Genk nilishauriwa kula vyakula vya sukari kwa sababu nilikuwa na fat nyingi mwilini”
VIDEO: Mechi ya Europa League ambayo Samatta aliihofia na kuhisi hahitajiki uwanjani