Jumamosi ys December 17 2016 timu ya Man United inayoongozwa na kocha wao mreno Jose Mourinho ilicheza mchezo wake wa 17 wa Ligi Kuu England dhidi ya West Bromwich Albion katika uwanja wa The Hawthorns.
Man United katika mchezo huo wa 17 wa Ligi Kuu wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-0, magoli yote yakifungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Sweden Zlatan Ibrahimovic dakika ya 5 na 56, ushindi huo unamfanya Zlatan kuweka rekodi.
Zlatan Ibrahimovic anakuwa amefikisha jumla ya magoli 152 ngazi ya vilabu toka kuanza kwa msimu 2011/2012 akiwa kafunga jumla ya magoli hayo akivichezea vilabu vya AC Milan ya Italia, Paris Saint Germain ya Ufaransa na Man United aliyojiunga nayo msimu huu akitokea PSG kama mchezaji huru.
https://youtu.be/37DCIkI_zMk
ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0