Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam kwa kushirikiana na Wananchi wa maeneo ya Gongo la Mboto wamewadhibiti Majambazi wawili waliokuwa na silaha ya moto baada ya kufanya tukio la uhalifu wa kupora fedha Tsh.Milioni 1.5 maeneo ya Chanika.
Hata hivyo, Majambazi hao akiwemo mmoja aliyefahamika kwa jina la Kulwa walifariki dunia wakati wanapelekwa Hospitali kupatiwa matibabu kutokana na kipigo walichokipata kutoka kwa Wananchi.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ACP Muliro Jumanne Muliro amesema tukio hilo limetokea October 26, 2022 saa 5:30 asubuhi ambapo Wahalifu hao walipora fedha hizo kutoka katika Kikundi cha Wakina Mama Chanika waliopewa fedha hizo kutoka Taasisi ya ASA.
“Ilipofika saa 5:30 asubuhi wakawa wamekusanya zile fedha zikawa zimefika Milioni Moja na Laki tano wakati wamekaa wakisubiri Mtu azichukue zile pesa wakatokea Majambazi wawili wakiwa kwenye pikipiki namba MC714CLL wakatishia kwa silaha wakapora zile pesa wakaondoka”