Serikali imetakiwa kutilia mkazo ujenzi wa vyumba maalum vya kujisitili wanafunzi wanapokuwa katika kipindi cha hedhi, ikielezwa elimu inayotolewa hasa matumizi wa Taulo za kike kuwawezesha kuhudhuria vipindi kwa asilimia kubwa hukwamishwa na miundombinu isiyo rafiki ya kuwawezesha kujihifadhi
Shule ya Sekondari Ngerengere Halmashauri ya wilaya ya Morogoro miongoni mwa Shule za Serikali zenye idadi kubwa ya wanafunzi, nako changamoto ni kubwa namna ya kujisitili wanafunzi wakike wanapokuwa kipindi cha hedhi.
Miongoni mwa jitihada zinazofanywa na uongozi wa shule kukabiliana na hali hiyo ni kuwa na angalau taulo za akiba, kuwawezesha wanafunzi kujisitili inapotokea kwa dharula.
Zipo pia jitihada zinazofanywa na wadau wa elimu, hapa mwakilisho kampuni ya utengenezaji na usambazaji wa Taulo za Kike ya Softcare Lucy Msami Pamoja na viongozi wengine wa kampuni hiyo wameifikia Shule ya Sekondari Ngerengere kuwawezesha Wanafunzi 480 Taulo za kike ,mahindi kilo 500 maharage kilo 200.
Mkuu wa wilaya ya Morogoro mbali na kupongeza jitihada za wadau hao amesema mpango serikali ni kuendelea kufanyia maboresho kuwa na miundombinu ya uhakika.
Hali hiyo namna ya kujisitili watoto wakike wakiwa katika kipindi cha hedhi ni changamoto kubwa kwa wanafunzi hasa maeneo ya vijijini, maeneo mengi hakuna kabisa miundominu wezeshi pia umbali kati ya shule na maeneo ya makazi.