Serikali imetoa Shilingi Bilioni 359.6 kukamilisha mradi wa Ujenzi wa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Msalato uliopo mkoani Dodoma.
Msimamizi wa mradi huo Corman Gaston amesema, fedha hizo zitatumika kwenye Ujenzi wa maeneo mbalimbali ya Uwanja huo.
‘Mradi huu unahusisha njia ya kurukia ndege (Runway) na sehemu ya kupaki ndege. Mradi huu utahusisha ujenzi wa fensi pamoja na miundonbinu mingine ya umeme, Pia utakuwa na uwezo wa kushusha ndege za kimataifa.” Amesema Gaston
Mradi huo wa ujenzi wa uwanja wa dege wa Kimataifa wa Msalato utakapokamilika utachochea uchumi wa Mkoa wa Dodoma pamoja na kukuza sekta ya Utalii.