Michezo ya Ligi Kuu England imeendelea leo Jumamosi ya February 4 2016 katika viwanja mbalimbali England, mchezo wa Arsenal dhidi ya Chelsea uliyochezwa katika uwanja wa Stamford Bridge ndio ulikuwa unasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka.
Mchezo huo wenye upinzani mkubwa katika jiji la London kutokana na kucheza kwa timu zinazotokea mji mmoja, umemalizika kwa Arsenal kukubali kufungwa kwa goli 3-1, magoli ya Chelsea yakifungwa na Marcos Alonso dakika ya 13, Eden Hazard dakika ya 53 na Cesc Fabregas huku goli la kufutia macho la Arsenal likifungwa na Oliver Giroud dakika ya 90.
Hicho kinakuwa kipigo cha 62 katika historia kwa Arsenal kufungwa na Chelsea katika michezo yao 189 waliyowahi kukutana, Arsenal wao wameifunga Chelsea mara 73 na sare mara 54, ushindi huo umeendelea kuiweka Chelsea katika nafasi nzuri katika mbio za kuwania Ubingwa wa EPL.
VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4