Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amewakata wakulima wa zao la Tumbaku nchini kujitokeza kwa wingi Kulima zao hilo kutokana na mpango wa sasa wa Serikali ni kuzalisha zaidi ya tani laki moja na elfu 30 ifikapo mwaka 2023.
Waziri Bashe ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya ya kutembelea viwanda vya uchakataji wa mazao ikiwepo kiwanda cha alliance One na kiwanda cha TLTC mkoani Morogoro ambapo amesema licha ya kuundwa kwa tume ya ufualiaji wa zao la Tumbuka bado kumekuwa na changamoto ya upatikani wa zao hivyo mpango wa Serikali ni kuhakikisha wakulima wananufaika na zao hilo.
Anasema Serikali ya awamu ya sita imejipanga kuzalisha tani laki moja na elfu 30 ili kuondokana na lawama ambazo zilikuepo kwa mda mrefu katika zao hilo la Tumbaku