Baada ya ushindi wa goli 1-0 waliyoupata Azam FC katika mchezo wao wa kwanza wa Kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Mbabane Swallows ya Swaziland, leo March 19 walicheza mchezo wao wa marudiano ugenini Swaziland baada ya mchezo wa kwanza kucheza Dar es Salaam.
Mchezo wa leo Azam FC ambao walitawaliwa na hujuma kutoka kwa wenyeji wao, walikuwa wakihitaji sare ya aina yoyote hata suluhu ili waweze kufuzu, bahati mbaya kwa Azam FC ni kuwa wamejikuta wakikubali kipigo cha goli 3-0 magoli yakifungwa na Sabelo Ndzinisa dakika ya 42, Wonder Nhleko dakika ya 68 na Sandile Hlatshwayo dakika ya 77.
Hata hivyo Azam FC ambao walikuwa wageni wa Mbabane walijikuta katika wakati mgumu kutokana na kufanyiwa fujo na mashabiki, kupigwa kwa mkurugenzi wao wa ufundi Saad Kawemba lakini kingine wachezaji walilazimika kuvalia ndani ya basi baada ya vyumba vya kubadilishia nguo kupulizwa dawa.
Kabla ya game AzamFC wakiwa Swaziland vs Mbabane walifanyiwa fujo uwanjani, dressing room zilipuliziwa dawa na walibadilishia nguo ktk gari. pic.twitter.com/JeVA3WRJt5
— millard ayo (@millardayo) March 19, 2017
ALL GOALS: Simba vs Yanga February 25 2017, Full Time 2-1