Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepiga kalenda kesi ya uchochezi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake.
Kesi hiyo iliyokuwa inasikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ambaye ameteuliwa kuwa Jaji, ilitajwa leo mbele ya Hakimu Mfawidhi, Kevin Mhina.
Wakili wa Serikali, Wankyo Simon ameieleza mahakama kuwa shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kutajwa na wana rufaa maalum ambayo bado haijasikilizwa, hivyo wanaomba ahirisho.
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Mhina ameahirisha kesi hiyo hadi February 14, 2019 kwa ajili ya kutajwa.
Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine ni Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko, Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Katibu wa Chadema, Dk. Vincent Mashinji, Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya na Katibu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu.
Wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya February Mosi na 16, mwaka huu maeneo ya Dar es Salaam.
ALIYEJENGA KABURI LA BILIONI 1 AZUNGUMZIA MAUAJI “WAMERUNDIKA VIUNGO, FREEMASON”