Naibu Waziri wa Mazingira Luhaga Mpina leo July 1, 2017 amewaagiza viongozi wote hasa Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanachukuwa hatua kali sana dhidi ya watu wasiofanya usafi katika mazingira yao na wanaotupa taka ovyo wakikiuka Sheria ya Utunzaji wa Mazingira.
“Kazi nzuri Watanzania mnafanya na mimi niwasisitize, niwaombe sana kwamba suala la kufanya usafi lisichukuliwe kama la hiyari. Ndiyo maana tunabadilisha Sheria zetu, tunaendelea kutunga Sheria ngumu zaidi ya kutaka watu wawe na mazingira yaliyo safi.
“Haiingii akilini ufanye biashara, uzalishe taka. Uko nyumbani kwako uzalishe taka, taka hizo unatupa ovyo, unafanya biashara unakusanya taka unatekeleza ovyo. Huwezi kuziondosha taka hizo, huwezi kufanya usafi wa eneo hilo halafu unataka mwenzako aje kufanya usafi kwenye eneo lako.
“Uzalishe taka wewe halafu sisi tuje tufagie nyumbani kwako? Hatuwezi kukubaliana na jambo hili. Naendelea kuwaagiza viongozi wote mnaohusika kuanzia Wakuu wa Wilaya kwamba chukueni hatua kali sana kwa Wananchi ambao wanafanya mambo hayo.” – Luhaga Mpina.
UVCCM walivyowajibu CHADEMA kuhusu kauli ya Mzee Mwinyi!!!