Siku moja baada ya kampuni ya udalali ya YONO Auction Mart ambao ni mawakala wa udalali wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA kuinyang’anya na kuishusha katika basi timu ya taifa ya vijana chini ya umri chini ya miaka 17 Serengeti Boys wakiwa njiani kuelekea katika mualiko wa chakula cha jioni na Makamu wa Rais.
Sports Extra ya Clouds FM imempata mkurugenzi wa huduma na elimu ya mlipa kodi wa TRA Richard Kayombo aelezee kuhusiana na suala hilo, ambapo Serengeti Boys walishushwa kutokana na deni la kodi la shirikisho la soka Tanzania TFF kutolipwa hadi sasa.
“Tunasikitishwa sana na kilichotokea lakini tuliagiza kampuni iliyofanya hivyo iliachie basi hilo mara moja na walifanya hivyo na tunafanya taratibu za kinidhamu kuhusiana na tatizo hilo na tutachukuwa hatua juu ya suala hilo kulingana na mkataba wetu na kampuni husika”
ALL GOALS: Taifa Stars vs Botswana March 25 2017, Full Time 2-0