Ni misimu mitatu sasa imepita toka Lionel Messi na Cesc Fabregas kutocheza katika timu moja baada ya Fabregas kurudi London kuitumikia Chelsea, licha ya kutocheza timu moja kwa misimu mitatu lakini urafiki wa Cesc Fabregas na Lionel Messi haujafa.
Lionel Messi na Cesc Fabregas bado wameendelea kuwa karibu na wamenaswa katika picha wakiwa na familia zao wana-enjoy katika fukwe za Hispania kipindi hiki cha mapumziko ya Ligi Kuu mbalimbali barani Ulaya.
Fabregas na Messi wametumia likizo zao pamoja katika kisiwa cha Balaeric Hispania, huku Lionel Messi akiwa na mama watoto wake Antonella Roccuzz na mwanae Thiago wakati Fabregas pia alikuwa na mpenzi wake Daniella Semaan pamoja na mtoto wake wa kike Lia.
VIDEO: Alichoamua Rais wa Simba baada ya kupokwa point 3 na TFF vs Kagera