Msanii ambaye ni mmoja ya matunda ya wasanii walioandaliwa vizuri na THT, Barnaba amesema aliwaza kufungua studio yake kama maktaba ya kuhifadhia muziki lakini akaenda mbali zaidi na kuona kama ana uwezo wa kuwaandikia wasanii nyimbo basi atumie studio yake pia ili kuwaandalia nyimbo zao.
Barnaba amefungua studio ambayo inaitwa ‘Hightable Records’ ambapo itawarahishia wasanii wanaotaka kufanya kazi na msanii huyo kuanzia kuandikiwa nyimbo mpaka kurekodi basi kazi yote itakuwa ikifanyika kwenye studio yake mpya.
Rapper Bonta anayewakilisha kundi la Weusi ambaye taaluma yake ya udaktari inamfanya awe pembeni ya jukwaa la muziki tofauti na wenzake leo ameachia ngoma mpya inayoitwa ‘Mauwongo Uwongo‘.
Bonta amesema ngoma hiyo inazungumzia uongo kwa ujumla, ameamua kufanya wimbo huo kwa sasa kutokana na kwamba tunaelekea kipindi cha uchaguzi ambapo wanasiasa wengi huongea uongo, hivyowimbo huo utawakumbusha wananchi wawe makini wasikubali kudanganywa na wanasiasa.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook