Juzi usiku club ya Singida United imetangaza kuingia mkataba wa miaka miwili na mshambuliaji wa kimataifa wa Rwanda aliyekuwa anaichezea timu ya Polisi FC ya Rwanda Danny Usengimana ambaye pia anaichezea timu ya taifa ya Rwanda.
Danny Usengimana aliibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu Rwanda mara mbili mfululizo na msimu uliyopita amefunga jumla ya magoli 19, usajili wake wa kujiunga na Singida United umeshitua wengi hususani baada ya stori za kusikia kuwa amesajiliwa kwa dola laki moja za kimarekani ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 200 za kitanzania.
Ayo TV ilifanikiwa kumpata mkurugezi wa Singida United Festo Richard Sanga atoe majibu kuhusiana na maswali wanaojiuliza wengi Singida United wanapata wapi fedha za usajili wachezaji kwa hela nyingi ukilinganisha timu walizopanda nazo daraja hazina uwezo kama wao.
“Tulijiandaa muda mrefu kufanya usajili lakini pesa tunatoa wapi za kufanya usajili huu ambao watu wengi wanatishika, kwanza wajue club inamilikiwa na mfanyabiashara wa madini ni mtu mwenye pesa zake, pili sisi tayari tumepata suporters na tuna wadhamini wanotusaidia” >>>Sanga
VIDEO: All Goals Taifa Stars vs Lesotho June 10 2017, Full Time 1-1