Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, SACP Fortunatus Musilimu amefanya ziara ya kushtukiza Kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo Mikoani na Nchi jirani, Ubungo na kuzindua uwekaji wa namba za simu kwenye mabasi kwa ajili ya abiria kutoa taarifa pale madereva wanapokiuka sheria za barabarani.
Kamanda Musilimu ameeleza kuwa hatua hiyo ni kusaidia abiria kutoa taarifa pindi madereva wanapokiuka sheria za Usalama Barabarani na kuhatarisha maisha yao na kusema zoezi hilo ni la nchi nzima ambalo litakuwa endelevu na ukaguzi wa mara kwa mara utafanyika kuhakikisha namba hizo hazitolewi kwenye mabasi hayo.
>>>”Abiria wazitumie kutoa taarifa kwa Kikosi cha Usalama Barabarani na yeyote atakeyehusika katika kuzitoa namba hizi kwenye mabasi atachukuliwa hatua kali za kisheria.” – Kamanda Musilimu.
Tazama kwa kuplay video hii jinsi IGP Simon Sirro alivyoshtukiza Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo na alichokifanya!!!